Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa acharuka nyumba 5 za walimu kujengwa kwa Mil. 500 - VIDEO

Video Archive
Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameshangazwa kupatiwa taarifa za ujenzi wa nyumba za walimu wa shule ya sekondari ya Iramba Wilaya Mufindi mkoani Iringa kujengwa kwa Sh milioni 100 na kuagiza kufanyika upya mapito ya gharama hizo.

Majaliwa ameyasema hayo leo akiwa mkoani Iringa kwa ajili ya ziara akiwa anazindua shule ya sekondari ya wasichana ya Iramba.

“Makadirio ya fedha inayokuja mnataka kujenga nyumba tano kwa Sh milioni 500 mwalimu hakuna nyumba ya Sh milioni 100 kwa mwalimu mmoja.

“Nyumba za walimu mmoja ni Sh. milioni 25 hadi 30 na tumejenga zipo hizo nyumba hiyo ni nyumba yenye vyumba vitatu, choo na eneo la stoo na kila kitu na ramani zipo nyie mnataka kujenga kwa ramani zipi” Waziri Mkuu majaliwa

Wakati akikagua madarasa pia ameagiza kuondolewa madawati yote ambayo hayana eneo la kuweka daftari kwa ajili ya wanafunzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live