Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa aagiza uchunguzi Luku

35334532b79e8678df077566d9f63093 Majaliwa aagiza uchunguzi Luku

Fri, 21 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza wafanyakazi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) waliosimamishwa kazi wasirudi kazini hadi uchunguzi utakapokamilika.

Majaliwa jana alimuagiza Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani kuwa meneja wa Tehama na wasaidizi wake wasisimamishwe kwa siku 10 tu kama ilivyotangazwa awali na kuagiza uchunguzi uendelee hadi utakapokamilika.

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa, Majaliwa alitoa agizo hilo alipozungumza na menejementi na Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco kwenye makao makuu ya zamani shirika hilo, Dar es Salaam jana.

“Lazima tufundishane kuwa makini, kila siku lazima tukague vifaa vyetu ili huduma ipatikane muda wote. Hakuna kuwasimamisha kwa siku 10, wakae pembeni hadi timu inayochunguza itakapotoa matokeo. Inawezekana sio wao tu, waziri endelea na uchunguzi.”

“Mmetengeneza usumbufu mkubwa sana, mlijua lazima kuwe na backup lakini hakuna, toka pale tulipoanza kutoa huduma mpaka leo kwanini hakuna backup, hilo ni jukumu lenu,” alisema.

Alisema serikali inataka kuona huduma ya umeme inapatikana muda wote na kwamba jitihada za kuimarisha vyanzo vya umeme zina lengo la kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa wingi na kwa gharama nafuu.

Juzi Dk Kalemani alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji Tanesco, Dk Tito Mwinuka amsimamishe kazi kwa siku 10 Meneja wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na Huduma za Biashara wa shirika hilo, Lonus Feruzi na wasaidizi wake wawili, Frank Mushi na Idda Njau.

Chanzo: www.habarileo.co.tz