Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa aagiza kigogo wilayani Nyang’hwale kusimamishwa kazi

29436 KASIMU+PIC TanzaniaWeb

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ofisa biashara Wilaya ya Nyang'hwale, Adam Nyoni kusimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhilifu wa Sh19milioni ambazo ni fedha za idara ya afya halmashauri ya Mbogwe.

Akizungumza na wananchi leo Alhamisi Novemba 29, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Masumbwe katika mji mdogo wa Mbogwe, Majaliwa ameonyesha kukerwa na tabia ya kuhamisha mtumishi mbovu na kumpeleka wilaya nyingine bila ya kumchukulia hatua.

Ameagiza uongozi wa Mkoa kumsimamisha kazi mara moja na kujibu tuhuma zinazomkabili.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz