Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Vita ya kudhibiti Ukimwi bado kubwa

29769 Majal%253Biwa+pic TanzaniaWeb

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imesema vita ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi bado ni kubwa na kutaka hatua zaidi zichukuliwe.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema hayo jana wakati akizindua Mkakati wa Nne wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi kwa mwaka 2018/19-2020/23 jijini hapa jana.

Majaliwa alisema mkakati huo pamoja na mambo mengine, utafanya mapitio ya mkakati wa awamu ya tatu wa taifa uliofanyika 2013/14-2017/18 na matokeo ya viashiria vya Ukimwi kwa 2016/17.

Alisema mkakati huo utapanga programu mbalimbali zitakazosaidia mwitikio wa Taifa zikiwemo za afua zinazotekelezwa kupitia mpango wa dharura wa Rais wa Marekani na Mfuko wa Dunia wa Kudhibiti Ukimwi.

Aliagiza mikoa yote kupeleka taarifa kwake ya namna walivyoadhimisha siku hiyo kabla ya mwisho wa mwaka huu.

“Kama nilivyosema katika uzinduzi wa ‘Furaha yangu’, utafiti wa nne uliofanyika ngazi ya kaya umeonyesha zaidi ya nusu ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) ndio walikuwa wanajua hali zao za maambukizi, naomba taarifa za kampeni hizi kutoka mikoani,” alisema Majaliwa.

Ukimwi, ugonjwa unaodhoofisha kinga ya mwili, uligundulika mwanzoni mwa miaka ya themanini miaka michache baadaye ulikuwa ushaenea mabara yote duniani. Ugonjwa huo hudhoofisha kinga za mwili na hivyo kuufanya ushambuliwe kirahisi na magonjwa mengine.

Akisoma taarifa ya wizara, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile alisema katika kipindi cha kuanzia Juni hadi Desemba 2018, Tanzania ililenga kupima watu zaidi ya 4.6 milioni ili kutambua afya zao, lakini waliopima hadi Novemba walikuwa 245,296.

Dk Ndungulile, ambaye pia alikiri kuwa mapambano dhidi ya Ukimwi bado ni makubwa kwa kuwa dawa haijapatikana, alisema kampeni ya “Furaha Yangu” imekuwa na mafanikio makubwa hasa kwa wanaume kujitokeza kupima.

Awali, mkurugenzi wa Tacaids, Dk Leonard Maboko alisema jumla ya watu 262,114 walipima afya zao katika kampeni ya “Furaha Yangu” iliyozinduliwa Juni 19, 2018

Kati yao, wanaume ni 125,725, sawa na asilimia 48 na na wanawake ni 136,389.

Dk Maboko alisema Mwanza inaoongoza kwa kupima watu 132,226, ikifuatiwa na Tabora (55,858) na Njombe (24,125).



Chanzo: mwananchi.co.tz