Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia asubuhi ya leo Jumatatu Novemba 12, 2018, kampuni 13 zimejitokeza kununua korosho.
Majaliwa amesema kati ya kampuni hizo, nane zimepeleka barua ofisi yake ya Dar es Salaam na tano zimepeleka Dodoma.
Amesema kampuni ya Mega Movers ipo tayari kuchukua tani 200,000 kwa bei ya Sh3, 000 na kampuni nyingine za Kitanzania zinataka kununua tani 5,000 kwa bei ya Sh3,500
Majaliwa amesema kuna viwanda vinane vinavyofanya kazi ya ubanguaji hawa tutawapa fursa.
“Wako Watanzania walidhani kwamba Serikali iliposema itanunua korosho walijua tutachukua fedha za kwenye bajeti hapana, tulishafanya tafiti kupitia Tantrade na balozi zetu,” amesema Majaliwa.
Endelea kufuatilia Mwananchi