Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Jiandaeni kwa Sensa, mtoe taarifa sahihi

4496b1fa058b507a93dabbc69293fb57 Majaliwa: Jiandaeni kwa Sensa, mtoe taarifa sahihi

Thu, 1 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kujiandaa na sense ya watu na makazi kwa kutoa taarifa zilizo sahihi huku akiwataka wakuu wa Mikoa, Wilaya na viongozi wengine kuanza kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi umuhimu wa sense.

Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni, akiharisha bunge la 12 ambapo alisema ni sense ya sita ambayo itasaidia serikali kupata taarifa za msingi. Sensa imepangwa kufanyika Agosti 2022.

“Sense hii itasaidia serikali kupata taaria za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya mamasuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo ya kimataifa.” alisema

Aidha Majaliwa ametoa wito kwa wito kwa watanzania wote kuanza maandalizi yatakayowezesha kutoa taarifa sahihi wakati wa sense hiyo ya watu na makazi huku wakitambua kuwa nsensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idada ya watu wote katika nchi kwa umri , jinsia na mahali wanapoishi.

Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo sense ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2021 . Bunge limehairishwa hadi Agosti 31, mwaka huu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz