Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Epukeni wanaotaka kuweka madini yetu rehani 

8c68c47f0ce29621bc377769f278798b Majaliwa: Epukeni wanaotaka kuweka madini yetu rehani

Sun, 4 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wa Isaka, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuwa makini na wagombea wanaojidani kuweka rehani madini ya Tanzania ili wapate fedha endapo watachaguliwa kuongoza nchi.

"Wanasema wataweka madini yetu rehani ili wapate fedha, sasa tukiwapa nchi, si watatuweka na sisi rehani?" alihoji.

Akasisitiza, "ndugu zangu msidanganywe, tarehe 28 twendeni tukamchangue Dk Magufuli, mbunge na madiwani wa CCM kwa sababu watatuletea maendeleo. Usipoteze muda, kwa mjomba hakuna urithi. Rudi nyumbani kumenoga," alisema.

Aliwata kumpigia kura Rais John Magufuli na madiwani wote wa CCM ambao wapo tayari kulinda rasilimali za nchi na kuwatumikia.

Pia amesema wawe tayari kutumia fursa ya ujenzi wa reli ya kisasa na ujenzi wa bandari kavu kujiletea maendeleo.

Alitoa mwito huo juzi wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa Kata za Kagongwa na Isaka akiwa njiani kuelekea Kata ya Kakola katika Jimbo la Msalala.

Alisema Isaka ni kitovu kikubwa cha biashara kwa sababu kuna miradi mikubwa miwili ambayo itatekelezwa.

Alisema kutakuwa na bandari kavu ambayo itakuwa inapokea mizigo kutoka nchi mbalimbali na akawataka wana Isaka kutumia fursa hiyo kufanya biashara.

“Wana Isaka tumieni fursa hii kujenga nyumba za kulala wageni na mahoteli ya kuuza vyakula,” alisema.

Alitaja reli ya kisasa itakayopita Isaka na kusema, ikikamilika, mtu atakuwa anatumia saa nne kwenda Dar es Salaam badala ya saa 14 ambazo zinatumika sasa kwa usafiri wa mabasi.

Majaliwa ambaye yuko mkoani Shinyanga kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli pia aliwanadi wagombea udiwani wa imbo la Msalala ambapo mgombea ubunge wa jimbo hilo, Iddi Kassim Iddi tayari ameshapita bila kupingwa.

Wakati huo huo, akizungumza na wakazi wa Kata za Segese na Kakola, Majaliwa alisema barabara ya kutoka Geita kupitia Kagongo hadi Kahama yenye urefu wa kilometa 106 itajengwa kwa kiwango cha lami.

"Barabara hii ilikuwemo kwenye ilani inayomalizika sasa uk.66 na ilipangiwa kufanyiwa upembuzi yakinifu lakini katika ilani yetu ya sasa, inatakiwa kukamilishwa ili wananchi muanze kufanya biashara kwa urahisi."

Akiwa jimbo la Shinyanga Mjini, Majaliwa alimwombea kura Rais Magufuli na mgombea ubunge, Patrobas Katambi.

Chanzo: habarileo.co.tz