Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaliwa: Amani imewezesha maendeleo nchini

2a913ae7c663ded69b43892fac8ae626 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuzingatia mahubiri ya viongozi wa dini ili nchi iendelee kuwa na amani ili maendeleo yaendelee kuonekana.

Aliyasema hayo leo alipohudhuria sala ya Ijumaa katika msikiti wa Buhari uliopo Ruangwa, mkoani Lindi. Waziri Mkuu amesema ni muhimu Watanzania wakajenga tabia ya kuaminiana, kuvumiliana pamoja na kupendana kwani mambo haya yote huchangia uwepo wa amani na utulivu.

"Nchi yetu imekuwa na kasi ya maendeleo katika maeneo mengi. Mimi naamini maendeleo haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na amani tuliyonayo na hii inatokana na mahubiri ya viongozi wetu wa dini. Dini ina mchango mkubwa sana katika uendeshaji wa Serikali," amesema

Chanzo: habarileo.co.tz