Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli awapiga chini RC Gambo, Madeni na Daqarro

3787 JPMs Magufuli awapiga chini RC Gambo, Madeni na Daqarro

Sat, 20 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo Juni 19, 2020 ametengua uteuzi wa viongozi watatu wa Mkoa wa Arusha na kufanya uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa zao.

Taarifa hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu amabayo inaeleza kuwa, Kwanza Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na amemteua Idd Kimanta kuwa mkuu wa mkoa huo.

Kabla ya uteuzi huo Idd Kimanta alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha na nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli itajazwa baadaye.

Kwa kutengua uteuzi wa pili na watatu unaweza kusoma kwenye barua hapo chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live