Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli ateua mwenyekiti, wajumbe bodi ya ushauri wa mapato ya mafuta na gesi

77392 MAGU+PIC

Fri, 27 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dk Leonard Chamriho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board).

Dk Chamriho ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Rais Magufuli amewateua wajumbe wanne wa bodi hiyo ambao ni;

  • Casmir Sumba Kyuki (Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria).

  • Dk Suleiman Magesa Missango (Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania – BOT).

  • Safiel Fahamuel Msomvu (Kaimu Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania – TPDC).

  • Dk Mussa Daniel Budeba (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM).

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Septemba 26, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania imemnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akisema uteuzi wa Dk Chamriho na wajumbe hao ulianza Septemba 25, 2019.

 

Pia Soma

Advertisement

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

26 Septemba, 2019

 

Chanzo: mwananchi.co.tz