Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli apigilia msumari suala la usajili wa meli nchini

1603 Nje 660x371

Sat, 20 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo January 19, 2018 President Dr. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume kusitisha usajili wa meli mpya hapa nchini mpaka itakapotangazwa vinginevyo.

President Magufuli ametoa agizo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere, kikao ambacho kimehudhuriwa na Mawaziri hao.

JPM amewaagiza Mawaziri hao pamoja na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kwa meli zote 470 ambazo zimesajiliwa hapa nchini na zinapeperusha bendera ya Tanzania.

“Kafanyeni uchunguzi wa kina kwa meli zote zinazopeperusha bendera ya Tanzania, fanyeni uchunguzi kwa meli zilizokamatwa ambazo ni 5 na pia hizi 470 zilizosajiliwa na zinazoendelea kufanya kazi, hatuwezi kuacha jina la nchi yetu lichafuliwe na watu wanaofanya mambo kwa maslahi yao” -Rais Magufuli.

President JPM ametaka maagizo yote yaliyotolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu kuhusiana na meli hizo yatekelezwe.

Pia President JPM amemuagiza Waziri Mahiga kuhakikisha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na Wakurugenzi wa idara za wizara hiyo wanafanya kazi zenye manufaa kwa nchi, ikiwemo kuwataka Mabalozi kutoa taarifa kila baada ya robo mwaka juu ya ukusanyaji wa.



“Wakupe taarifa kila baada ya robo mwaka, na Balozi ambaye atakuwa hakusanyi mapato vizuri na kuinua biashara na uwekezaji atakuwa hafai kuendelea kuwa Balozi, tena kawaambie kabisa kwenye suala hili hakuna mchezo” – Rais Magufuli.

JPM amemtaka Waziri Mahiga na watendaji wa wizara yake kufuatilia kwa ukaribu na kushirikiana na Mawaziri wanaohusika katika utekelezaji wa mikataba ambayo Tanzania imetiliana saini na nchi nyingine na kwamba hataki kusikia utekelezaji wa mikataba ambayo baadhi yake inahusisha miradi mikubwa yenye manufaa kwa Tanzania, unakwama ama kusuasua.

“Mnapokuwa mnahitaji taarifa kutoka wizara nyingine kama ni Waziri muandikie Waziri mwenzako kama ni Katibu Mkuu muandikie Katibu Mkuu mwenzako halafu nakala ya barua ilete kwangu kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, nataka nione huyo atakayechelewesha ama kutotoa taarifa” -Rais Magufuli.

GARI YA FFU IMEPINDUKA KUTOKANA NA MWENDOKASI IMEUA ASKARI 2, KAMANDA MPINGA AMEONGEA



 

 

Chanzo: millardayo.com