Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli ampa Waziri Simbachawene wiki moja "hakuna kinachoshindikana" (+video)

Video Archive
Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amempa siku saba Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, ahakikishe wastaafu wote wa jeshi la polisi wanaodai mafao yao wanalipwa ndani ya siku hizo.

Rais Dkt. Magufuli ametoa maagizo hayo akizungumza na Askari Polisi mara baada ya kuzindua Chuo cha Maafisa wa Polisi Kurasini DSM, ambapo awali IGP Sirro alimuomba Rais Magufuli awasaidie wastaafu ambao hawajalipwa mafao yao waweze kulipwa kwa wakati.

“Waziri Simbachawene nakuagiza nenda kashughulikie malipo ya wastaafu na ikiwezekana ndani ya wiki moja wawe wamelipwa, tuliwatumia vizuri wakati hawajastaafu ni lazima wafaidike na kustaafu kwao hakuna kinachoshindikana pesa ipo,” Rais Dkt. Magufuli.

Chanzo: millardayo.com