Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli aliniahidi pesa na uwaziri - Msigwa

Msigwa Magufuli Magufuli ana Msigwa.

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kada wa Chama cha Demokrasia ambaye alikuwa anagombea Uenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, na mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema aliwahi kushawishiwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli ili ahamie Chgama Cha Mapinduzi (CCM).

Mchungaji Msigwa amedai kuhujumiwa katika mchakato huo uliogubikwa na vitendo vya rushwa.

"Kwani mimi nikitaka kuhama chama kuna mtu anaweza kunizuia? Kwani lazima nilete figisu si naaga tu navaa nguo kama naende kanisani au ACT. Mimi nina independent mind vile ambavyo nilikuwa naweza kumkosoa Hayati Magufuli kwenye serikali yake na chama changu kikifanya makosa kitakosolewa hivyohivyo.

"Magufuli alisema njoo utapewa ubunge, utapewa hela na nitakupa uwaziri na nyie mliona magari yamekuja pale Segerea yamenifuata nikakataa ananipa simu msaidizi wake nikakataa, unamkatalia Rais kweli wewe, nitajie wa siku hizi hawa wakiitwa na Rais wanatoka mbio," amesema Msigwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live