Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli, Mnangagwa wakubaliana kuimarisha biashara na uwekezaji

10375 MNAGA+PIC TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa wamekubaliana kuimarisha biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili.

 

Hayo yameelewa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Ijumaa Juni 29, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa viongozi hao wamefikia makubaliana hayo baada ya kufanya mazungumzo rasmi na baadaye kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, Ikulu jijini hapa.

 

Akimnukuu Rais Magufuli, taarifa hiyo imesema kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa na thamani ya Sh18.3bilioni na mwaka 2017 ilikuwa Sh21.1bilioni, mpaka sasa Zimbabwe imewekeza nchini zaidi ya Sh72.2bilioni, kiwango ambacho ni kidogo ikilinganisha na uhusiano wa mataifa hayo.

 

Kutokana na hali hiyo, Rais Magufuli amesema wamekubaliana kuwa na tume ya  pamoja ya ushirikiano ambayo mara ya mwisho ilikutana mwaka 1998, kutaka ikutane tena baada ya uchaguzi mkuu wa Zimbabwe utakaofanyika Agosti, 2018 ili kusaka jibu la kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo.

 

“Nakushukuru Rais Mnangagwa kwa kukubali mwaliko wa kuja kutembelea hapa Tanzania ikiwa ni miezi 6 tangu uingie madarakani na ukiwa  katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu,” amesema Rais Magufuli.

 

“Nakupongeza kwa namna unavyochukua hatua ikiwamo kuimarisha demokrasia, kukuza uchumi na kumpa heshima Baba wa Taifa la Zimbabwe, rais mstaafu Robert Mugabe.”

 

Kwa upande wake Mnangagwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kumualika na amesisitiza kuwa Zimbabwe inatambua mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Taifa hilo pamoja na mataifa mengine ya Afrika ambayo yaliendesha harakati zao za ukombozi nchini Tanzania.

 

Amemuahidi Rais Magufuli kuwa nchi yake ipo tayari kukuza ushirikiano wake na Tanzania katika kuimarisha biashara na uwekezaji hususani katika kilimo, utalii, usafiri wa anga, madini pamoja na ulinzi na usalama.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz