Dodoma. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, Angelina Mabula amesema Serikali ilitoa mkopo usio na riba kwa halmashauri 24 nchini lakini ni halmashauri nne tu ndizo zilizotekeleza.
Mabula ameyasema hayo leo Alhamisi Februari 13, 2020 katika uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma uliozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Amesema halmashauri hizo zilipewa mkopo wa Sh6.2 bilioni,
“Sababu kubwa ya kutotekeleza kwa halmashauri hizo ni kutokuwa waaminifu.”
Amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Mbeya, Kahama, Ilemela na Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amemuomba Majaliwa kutoa motisha kwa wawekezaji katika jiji la Dodoma.
Pia Soma
- TRA wakamata bidhaa za mamilioni kutoka Kenya
- Bavicha kutumia siku wa wapendanao kuhamasisha uandikishaji daftari la wapiga kura
- Watumia zebaki bila kujali athari watakazopata
Hoja hiyo iliyoungwa mkono na Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM), Anthony Mavunde aliyesema kuendelea kwa jiji la Dodoma kunahitaji ushirikiano kati ya Sekta binafsi na Serikali.
Ameiomba Serikali kutumia Sheria ya mwaka 1989 ambayo ilitoa unafuu kwa wawekezaji.
Amesema kitendo cha mpango huo kutogusa kuhamisha wakazi 4,000 wa kata ya Mtumba jijini hapa kumewafanya wakazi wa eneo hilo waliokuwa na hofu kumalizika.