Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene, amelitaka jeshi la polisi mkoa wa Arusha kutoa huduma nzuri kwa wananchi ili waweze kujenga imani kubwa kwa jeshi hilo kwani wao ndiyo wenye mamlaka ya kuleta amani kwa jamii au mitafaruko.
Kauli hiyo ameitoa akiwa kwenye ziara yake mkoani Arusha, na kulipongeza jeshi la polisi Karatuu kwa kufanya kazi nzuri ya utoaji huduma kwa wananchi.
“Jeshi la polisi na ‘nature’ ya kazi yake linaweza kusababisha amani ama kuvuruga amani katika jamii kwa sababu nyie ndiyo mnaoishi na watu na kila mahali ambapo wapo raia na askari polisi wapo ndiyo maana hata lawama huwa zinasikika sana kuliko mema na mazuri mnayoyafanya ni kwa sababu kila mahala mpo,” Waziri Simbachawene.
Mbali na hayo Waziri Simbachawene, amewataka Askari hususani wale wanaokuwa katika vituo vya utalii kuwa kioo kwa watalii waoingia nchini ili waweze kuitangaza Tanzania katika mataifa mengine.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATOA MAAGIZO “MNAWEZA KUVURUGA AMANI,WALETWE HAPA”