Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maagizo ya Bunge wanaopiga muziki kwenye makazi ya watu

Zungu Er Maagizo ya Bunge wanaopiga muziki kwenye makazi ya watu

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu amelielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufuatilia na kutoa adhabu kali kwa wanaopiga kelele za muziki bila kufuata kibali cha NEMC katika maeneo ya makazi ya Watu.

Zungu ametoa maelekezo hayo wakati wa kuhitimisha mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambapo Bungd limepitisha makadirio ya Tsh. Bilioni 54.1 kwa ajili ya matumizi kwa mwaka 2023/24.

“Suala la makelele kwenye maeneo ya Watu limezidi Watu wanakereka, Watu wanaugua Wazee wengi wanateseka sana na makelele ya muziki wala haina control yoyote kwahiyo NEMC mlifuatilie na mtoe adhabu kali kwa wanaokiuka taratibu za uchafuzi wa mazingira hasa kwenye makelele,” amesema Zungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: