Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LIVE: Rais Samia akiwaapisha Mwigulu Nchemba na mawaziri wengine

Video Archive
Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza la mawaziri, Rais Samia Suluhu Hassani, leo Julai 14, 2023 anawaapisha wateule hao wapya akiwemo Mwigulu Nchemba ambaye wizara yake ilipunguziwa majukumu na kubaki kuwa Wizara ya Fedha pekee.

Awali, wizara hiyo ilikuwa ikitambulika kama Wizara ya Fedha na Mipango.

Julai 5, 2023, Rais Samia alifanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na kuunda wizara mpya.

Rais Samia alivunja Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuunda Wizara tatu; Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Katika Mabadiliko hayo, alimteua aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.

Pia alimteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji ofisi ya Rais.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live