Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusaga: Nilikuwa napiga muziki nyumbani kwa Mengi

56103 Kusagapic

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema amemfahamu aliyekuwa mwenyekiti wa kampuni za IPP, Reginald Mengi miaka 26 iliyopita na alikuwa akienda nyumbani kwa mfanyabiashara huyo kupiga muziki.

Akizungumza leo Jumanne Mei 7 katika viwanja Karimjee ambako watu wa kada mbalimbali wanaaga mwili wa mfanyabiashara huyo, Kusaga amesema katika shughuli hiyo alikuwa akizungumza na marehemu mambo mengi ikiwamo mipango ya kuanzisha radio.

Kusaga amesema Mengi alikuwa ni mtu ambaye anaweza kujishusha na kuzungumza na vijana kana kwamba analingana nao umri.

“Mimi nilikuwa nazungumza naye tunapiga stori kabisa, kiukweli ni kwamba taifa limepoteza mtu, Moat (Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari) imempoteza kiungo muhimu na kuziba nafasi yake itabidi ifanyike kazi kubwa.”

“Yeye alianza kufungua radio lakini alikuwa akinipa mawazo na njia za mimi kuweza kuanzisha radio, hebu fikiria mtu una chombo cha habari halafu unamuelekeza mwingine jinsi ya kuanzisha chombo kama hicho,” amesema Kusaga.



Chanzo: mwananchi.co.tz