Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ni miongoni mwa viongozi walioudhuria katika Azimio la Kagera lililozinduliwa December 16, 2017, ambapo amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanayatumia vyema mawazo ya vijana.
“Mawazo mazuri ya hawa vijana na watu wengine tunayoyajadili hayatoweza kufanikiwa kama viongozi wa serikali na hasa watendaji watashindwa kubadilisha mitazamo yao, kuna watu wamekaa maofisini wanajifanya kama miungu watu,” – Waziri Jafo
“Wakurugenzi maazimio tunayotoka nayo hapa leo, lengo lake kubwa ni kuipeleka nchi yetu mbele, mchukue mawazo mazuri tuzibadilishe Halmashauri zetu, Watanzania wote hakuna anayeishi hewani kila Mtanzania anaishi katika Vijiji na Mitaa, niwaagize wote waende wakatimize wajibu wao,” – Waziri Jafo
RUGE “YAWEPO MAZUNGUMZO KATI YA MAPROFESA NA WAHITIMU WA DARASA LA 7 WENYE UZOEFU” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA