Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa kunyimwa unyumba amuua Mkewe

Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoani Njombe, Mahamoud Banga Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Njombe, Mahamoud Banga amesema chanzo cha mtuhumiwa wa mauaji, Juma Kyando kwa mke wake, Tumaini Luvanda (35) ni ugomvi wa kifamilia wa muda mrefu uliosababishwa na kunyimwa tendo la ndoa.

Mwanaume huyo anadaiwa kumuua mke wake kwa kumkatakata viungo vyake kisha kuvitia kwenye mfuko na kuvitupa kwenye mto ulio jirani na nyumba yake eneo la Kabinda mkoani humo.

Akisimulia tukio hilo Kamanda Banga amesema siku ya tukio marehemu alichelewa kurudi na alipoulizwa na mume wake hakutoa maelezo mazuri na ndipo mume huyo alipopandwa na hasira na kisha kutekeleza tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live