Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipanya azitaka Bilioni 5 kwa Mwijaku, kesi kusikilizwa Septemba 3

Video Archive
Thu, 8 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji, Masoud Kipanya amemfungulia Mtangazaji mwenzake Mwemba Burton almaarufu ‘Mwijaku’ kesi ya madai ya udhalilishaji kupitia mitandao ambapo ameiomba Mahakama Kuu imwamuru Mwijaku amlipe Fidia ya Tsh. Bilioni 5.5 na gharama nyingine za Kesi.

Mnamo Juni 2024 kupitia Mitandao ya Kijamii Mwijaku alidai Masoud anafanya biashara haramu na amekuwa akihongwa kuwasema vibaya Viongozi na Serikali.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Septemba 3, 2024, na Mwijaku amepewa wito kufika Mahakamani na kuwasilisha utetezi ndani ya siku 21.

Pia, atatakiwa kulipa 31% ya riba ya Fidia ya Madhara Halisia tangu alipotoa kashfa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live