Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Ugaidi:Mbowe asomewa upya mashtaka, wakili afunguka (Video+)

Video Archive
Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabil Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe imeahirishwa hadi August 13, 2021 kwa ajili ya Upande wa Mashitaka kuwasilisha taarifa za kesi hiyo kutoka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Hata hivyo, mshtakiwa Mbowe na wenzake watatu wamesomewa upya mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambayo ni kula njama na tuhuma za Ugaidi ambayo waliyatenda kati ya Mei 1 na August 1, 2020 maeneo ya Moshi, Dar es Salaam, Morogoro na Arusha.

Mbowe alifikishwa kwa mara ya kwanza July 26, 2021.

“Leo mnamo tarehe 6 Agosti 2021 Freeman Mbowe pamoja na washtakiwa wanne wamesomewa upya mashtaka  kwa mujibu wa  Sheria kwa ujumla Freeman Mbowe anashtakiwa kwa kula njama za kutenda vitendo vya kigaidi ni kwamba alikula njama katika hotel moja uko Moshi za kutenda makosa ya kigaidi vya kufanya ulipulizi wa vituo vya mafuta”- Wakili Peter Kibatala

Chanzo: millardayo.com