Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mbowe, Mahakama Yakataa Mapingamizi ya Serikali - Video

Video Archive
Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kesi ya Mbowe, Mahakama Yakataa Mapingamizi ya Serikali – Video August 30, 2021 by Global Publishers



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Agosti 30, imeanza kusikiliza Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Mahakama Kuu kanda ya DSM chini ya Jaji John Mgetta imetupilia mbali mapingamizi manne yaliyowasilishwa na Jamhuri katika kesi Na. 21/2021 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe.

Kesi hiyo itasikilizwa kuanzia Septemba 06, 2021 kwa njia ya maandishi na hukumu kutolewa Septemba 23, 2021.Aidha, Kesi ya Mbowe anayokabiliwa na mashtaka ya ugaidi inatarajiwa kuendelea kesho Jumanne, Agosti 31, 2021 katika Mahakama Kuu – Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu (maarufu kama Mahakama ya Mafisadi) iliyopo katika Chuo cha Sheria, Ubungo Mawasiliano jijini Dar es Salaam.

Chanzo: globalpublishers.co.tz