Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Rais Samia juu Katiba Mpya, mikutano ya hadhara (+video)

Video Archive
Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kumpa muda aimarishe uchumi wa nchi ili aweze kuangalia suala la Katiba Mpya na mikutano ya hadhara ambayo kwa sasa imezuiwa.

“Kama inavyosemwa nimeanza vizuri naomba nipeni muda nisimamishe nchi kwanza kiuchumi. Tuite wawekezaji wawekeze ajira zipatikane uchumi ufunguke halafu tutashughulikia Katiba, tutashughulikia mikutano ya hadhara wakati ukifika.” Rais Samia 

“Kwa sasa tunaruhusu mikutano ya ndani ya vyama  na wabunge wapo huru kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao si maeneo ya wengine…, ile yeyeee ingieni…, hili naomba sana Watanzania tujipe muda tufanye uchumi wetu…, sisemi katiba si ya maana lakini naomba mnipe muda kwanza nisimamishe uchumi kisha tutatizama mengine,”  Samia.

“Sasa hivi nchi yetu ina changamoto nyingi sana, kuna janga la corona, uchumi umeshuka tunatakiwa kuupandisha. Na hili nataka niliunganishe na lile la Katiba Mpya. Kuna mambo mengi ya kushughulikia, nimesema ninakwenda kuifungua nchi kwa sababu uchumi umeshuka tunatakiwa kupandisha uchumi, tukifungua nchi.”

Chanzo: millardayo.com