Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kadi za mpiga kura za mwaka 2015 na 2020 ni halali

Kura Msjzkzk Kadi za mpiga kura za mwaka 2015 na 2020 ni halali

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhan amesema kadi za mpiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 ni halali na zitaendelea kutumika kwenye chaguzi zijazo, bila kujali mabadiliko ya jina la tume ya uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Kailima amesema hayo leo Jumatatu, Julai 22, 2024 wakati wa ziara ya kukagua vituo vya kuandikishia wapiga kura katika Halmashuari ya Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

“Naomba nitoe wito kwa wale ambao kadi zao ni zile zenye jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wanadhania kubadilika kwa jina la tume kunasababisha kubadili kadi watambue kadi zao ni halali kwa mujibu wa kifungu cha 168 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024,” amesema.

Kailima amewakumbusha wananchi wa mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi kuwa zimebaki siku tatu kazi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kukamilika kwenye mikoa yao, hivyo ni muhimu kujitokeza kwa wingi na kutumia vizuri siku hizo.

Uboreshaji wa Daftari kwenye mikoa hiyo ulianza Julai 20, 2024 na utafanyika kwa siku saba hadi Julai 26, 2024. Vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live