Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kabendera atiwa hatiani kwa mashtaka mawili

Video Archive
Wed, 26 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu nchini Tanzania  imemtia hatiani mwandishi wa habari , Erick Kabendera.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo Jumatatu Februari 24, 2020 baada ya Kabendera  kukiri mashtaka yake mawili ya  kukwepa kodi na kutakatisha Sh173 milioni.

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya upande wa mashtaka kumsomea maelezo ya awali ya mshtakiwa huyo.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu

Leo amefutiwa shtaka la kuongoza genge la uhalifu na kubaki na mashtaka mawili ya  kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz