Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joel Lwaga awatoa machozi waombolezaji mazishi ya Mengi

56106 Mengipic

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wimbo wa ‘Sitabaki nilivyo’ ulioimbwa na msanii, Joel Lwaga umewatoa machozi baadhi ya waombolezaji waliofika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa  mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi.

Ameimba wimbo huo leo Jumanne Mei 7 baada ya Rais John Magufuli na viongozi wengine wa Serikali kuaga mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu atakayekumbukwa kwa misaada mbalimbali kwa jamii aliyoitoa enzi za uhai wake kwa watu wa kada mbalimbali.

Wakati wimbo huo ukiendelea baadhi ya waombolezaji walionekana wakitikisa vichwa huku wakiwa na sura za huzuni, wengine wakitoa vitambaa kwenye mifuko yao na kujifuta machozi.

Shughuli ya kutoa heshima za mwisho bado inaendelea katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wastaafu na wananchi.



Chanzo: mwananchi.co.tz