Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi Lowassa alivyomzungumzia Mengi

56283 Pic+lowasa

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Reginald Mengi akimwelezea mwenyekiti mtendaji huyo wa IPP kuwa alikuwa kielelezo cha mtu aliyechukia umasikini.

Taarifa ya Lowassa iliyotolewa leo Jumatano Mei 8 na Aboubakary Liongo ambaye ni msemaji binafsi wa mwanasiasa huyo imesema: “Kwa majonzi makubwa naandika kumlilia kaka na rafiki yangu Dk Reginald Mengi aliyefariki dunia.”

“Dk Mengi alikuwa kielelezo halisi cha mtu anayechukia umasikini kwa vitendo na kuishi maisha yake kuwanyanyua wengine katika kuupinga umaskini.”

“Umekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya taifa letu na watu wake. Umeacha alama kubwa ya upendo, moyo wa kutoa na unyenyekevu kwa jamii alama ambayo Watanzania tutakukumbuka nayo daima. Lala salama kaka,” amesema.

Mengi aliyefariki dunia Mei 2 akiwa Dubai, Falme za Kiarabu, alizaliwa Mei 29, 1942.



Chanzo: mwananchi.co.tz