Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inasikitisha: Mtoto anakula kwa kutumia mguu, amuomba Rais Samia amsaidie

Video Archive
Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika Kaya za Vijijini imekuwa ni kawaida kwa Wanafunzi kufaulu na kushindwa kuendelea na masomo kisha kubaki nyumbani kutokana na ugumu wa maisha unaopelekea kushindwa kukidhi mahitaji ya shule huku wengine wakiacha kuendelea kutokana na kutopata msukumo kutoka kwa wazazi wao au kupewa majukumu mengine kama kuchunga N'gombe na kulima.

Jambo hilo limepekea Polisi Kata wa Kata ya Mtimbira, Wilaya ya Malinyi katika Mkoa wa Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Henry Mwangake kupita katika kaya ambazo zina wanafunzi waliofaulu kidato cha nne na kushindwa kuendelea kutokana na changamoto mbalimbali kwa lengo la kuwahamasisha au kuwatafutia wadau ili waweze kupata msaada kwa wenye uhitaji.

Akiwa nyumbani kwao Kijana Hamisi Nguku mlemavu wa mikono na miguu anayetumia mguu kuandika ambaye amefaulu kidato cha nne na kushindwa kuendelea na kidato cha tano kutokana na ugumu wa maisha.

Mkaguzi Mwangake amesema, Kijana huyo mlemavu mwenye kipaji cha uchoraji amefaulu kwenda kidato cha tano lakini ameshindwa kwenda kutokana na ugumu wa maisha hivyo ameomba mdau yeyote atakayeguswa aweze kurudisha tabasamu la mtoto huyo kwa kumlipia mahitaji ya shule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live