Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inasikitisha! Mama ajifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa, inauma-VIDEO

Video Archive
Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: Global Tv

Rukia Mohamed, mama mmoja nchini Tanzania mwenye umri wa miaka 25 anahitaji msaada wa kila namna baada ya kumzaa mtoto mwenye ulemavu na maumbile yasiyo ya kawaida.

Mama huyo ambaye alikuwa anazungumza na runinga ya Global Tv alisema kuwa mtoto huyo ni wake na wala hakubadilishiwa kwani kipindi akiwa mjamzito, daktari baada ya vipimo vya ‘scanning’ alimwambia kuwa kijusi chake kitakuwa na ulemavu.

Katika video hiyo ya mazungumzo marefu, mtoto huyoanaonekana kutokuwa wa kawaida, akiwa na kichwa kikubwa kuzidi kawaida, sehemu zingine za mwili zikiwa dhaifa na unyonge huku usoni, mdomo ukiwa kama wa sungura.

“Miezi sita ilivyotimia nilienda kufanya vipim vya pili, wakaniambia kuna dalili ambazo zinaonesha kuwa utazaa mtoto mwenye ulemavu. Nilimkuta ni yule sijabadilishiwa wala hawakunidanganya,” mama mtoto alieleza.

Swaleh Mng’ola, ambaye ni mume wake na baba mtoto huyo alisema kuwa hayuko tayari kumkimbia kwani si kosa lake na hakuna aliyechagua yule mtoto kuzaliwa na maumbile hayo ya ajabu.

“Yule mtoto kwa vile si mtoto aliyechagua wala si makosa ya mama. Yale ni maumbile kwa hiyo ni mipaango ya mwenyezi Mungu. Yule mtoto kazaliwa vile kwa hiyo hata yeye hajapenda na hata mamake hajapenda kwa hiyo siwezi kumkimbia kwa sababu ni jambo limetokea kwa kukusudia isipokuwa ni mipango ya Mungu,” Mng’ole alisema.

Rukia alisema kuwa alimchukua mtoto yule kwa vipimo vya MRI kichwani lakini akaambiwa kuwa mtoto hawezi kufanyiwa upasuaji katika umri huo kwani maji yalikuwa mengi na ubongo kidogo.

Alisema kuwa mtoto huyo kutwa nzima Analia na wala hajajua Analia kutokana na maumivu au njaa.

Famlia hiyo sasa inaomba msaada wa chochote kitu ili mtoto wao wa kike kufanyiwa matibabu na angalau kuona kama hali yake inaweza kurejea kama ya mtoto wa kawaida.

“Tunaomba mtu yeyote ambaye anaguswa na tukio hili aweze kutusaidia kwa njia yoyote ile ili tuweze kupata matibabu kwa huyu mtoto, Susan Bima,” baba mtoto alitoa wito.

Chanzo: Global Tv