Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibada ya Kuaga Wanafamilia 5 Waliofia Uwanjani Wakimuaga JPM - Video

Video Archive
Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Ibada ya Kuaga Wanafamilia 5 Waliofia Uwanjani Wakimuaga JPM – Video March 25, 2021 by Global Publishers



MAJONZI na simanzi vimetawala leo Alhamisi, Machi 25, 2021, kwa waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki wakati wa ibada ya kuaga na zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa miili ya wanafamilia watano wa Kimara mkoani Dar es Salaam waliofariki pamoja.



Ndugu hao wanadaiwa kufariki Machi 21, 2021, katika Uwanja wa Uhuru kutokana na msongamano walipokwenda kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Mbunge wa Kibamba (CCM), Mtemvu Issa amewasili kwenye msiba huo leo Alhamisi, kutoa pole kwa familia hiyo.



Waliofariki dunia ni Susan Mtuwa na watoto wake wawili, Nathan (6) na Natalia (5) pamoja na watoto wengine wawili Cris (11) na Michelle (8) ambao ni watoto wa shemeji zake Susan huku dada wa kazi wa familia hiyo aliyekwenda pamoja nao uwanjani hapo.



Wakati hayo yakielezwa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alieleza kuwa katika shughuli hiyo baadhi ya watu walijeruhiwa lakini hakuna na idadi kamili.

Jumatatu, Machi 22, mchana ofisi ya habari na uhusiano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ilitoa taarifa ya kupokea majeruhi saba na maiti moja. Kati ya majeruhi hao mmoja aliruhusiwa kurejea nyumbani.



Kuhusu vifo hivyo, kaka mkubwa wa familia hiyo, Gerald Mtuwa amesema kuwa Suzan aliondoka na watoto hao saa 11 alfajiri pamoja na dada wa kazi ambaye hadi Jumatatu hakujulikana alipo.
Chanzo: globalpublishers.co.tz