Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

IGP awaita vijana waliomba ajira jeshi la polisi

IGP Awaita Vijana Waliomba Ajira Jeshi La Polisi.png IGP awaita vijana waliomba ajira jeshi la polisi

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Jeshi la Polisi anapenda kuwatangazia kuwa vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi kupitia mfumo wa Ajira TANZANIA POLICE FORCE RECRUITMENT PORTAL, usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 29/7/2024 hadi tarehe 11/8/2024 nchini kote.

Waombaji wa Tanzania Bara wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) kilichopo Barabara ya Kilwa (Kurasini).

Waombaji wenye elimu ya kidato cha nne na sita usaili wao utafanyika kwenye mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.

Waombaji wa Zanzibar wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na nne usaili utafanyika Zanzibar. Kwa walioko Mikoa ya Unguja usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na Mikoa ya Pemba usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).

Kila mmoja anatakiwa kufika akiwa na vyeti halisi vya taaluma (academiccertificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mamlaka ya Utambulisho wa Taifa NIDA au namba ya utambulisho wa Taifa NIDA, nguo na viatu vya michezo.

Kijana yeyote atakaefika kwenye usaili baada ya tarehe 29/07/2024 hatopokelewa. Orodha ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili imeambatishwa pamoja na tangazo hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live