Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndiye Dk Hussein Ali Mwinyi

Ded5672eeb923051fe74e4a920b65a8f Huyu ndiye Dk Hussein Ali Mwinyi

Mon, 2 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Dk Hussein Ali Mwinyi (53) ameampishwa leo Saa 4 na dakika 50 katika Uwanja wa Amaan, Unguja, Zanzibar na kuchukua nafasi ya Rais Ali Mohamed Shein ambaye muda wake umemalizika.

Dk Shein amemaliza awamu mbili za uongozi wake ndani ya Serikali ya Zanzibar ambayo alianza kuitumikia Novemba 03, 2010.

Dk Mwinyi ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ameapishwa kuwa Rais wa awamu ya nane wa Zanzibar baada ya kuwashinda katika kinyang’anyiro cha Urais wapinzani wake akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad aliyewania kiti hicho kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Rais Mwinyi alishinda kinyang’anyiro hicho kwa kupata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27dhidi ya mpinzani wake mkuu Maalim Seif aliyepata asilimia 19.87 katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 na 28, mwaka huu

WASIFU WA DK HUSSEIN ALI MWINYI:

Dk Mwinyi alizaliwa Desemba 23 mwaka 1966, na ni mtoto wa Ali Hassan Mwinyi, aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar kisha Rais wa Tanzania kati ya mwaka 1985 hadi 1995.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Julai 10 mwaka huu 2020, kilimchagua Dk Mwinyi ambaye hapo awali alikuwa Waziri wa Ulinzi wa Tanzania kuwa mgombea urais wa Zanzibar, na kuwashinda watia nia 31 waliojitokeza kuwania kupeperusha bendera ya chama kwenye nafasi hiyo kubwa zaidi katika Serekali ya Mapinduzi Zanzibar.

Akiwa na umri wa miaka 53 kwa sasa, Dk Mwinyi amewahi kuhudumu kama Naibu Waziri wa Afya, Waziri wa Nchi Muungano, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, na Wazira wa Ulinzi ambayo amehudumu kwa miaka tisa hadi anaingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais.

Mwinyi alitangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya urais Oktoba 29, 2020 baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Hamid Mahmoud Hamid kumtangaza kushinda kwa kupata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27 ya kura zote 382,402.

MARAIS WASTAAFU ZANZIBAR

Dk. Mwinyi anakuwa Rais wa nane tangu kufanyike Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 1964 akipokea kijiti kutoka kwa Dk Shein ambaye ni mstaafu.

Marais waliopata kuongoza Zanzibar ni ; Abeid Karume (26 Aprili 1964- 7 Aprili 1972), Aboud Jumbe (7 Aprili 1972- 30 Januari 1984), Ali Hassan Mwinyi (30 Januari 1984- 24 Oktoba 1984), Idris Abdul Wakil (24 Oktoba 1985- 25 Oktoba 1990).

Salmin Amour (25 Oktoba 1990- 8 Novemba 2000), Amani Abeid Karume (8 Novemba 2000- 3 Novemba 2010) na Dk. Ali Mamohed Shein aliingia 3 Novemba 2010 hadi leo Jumatatu anapokabidhi madaraka kwa Dk. Mwinyi.

Chanzo: habarileo.co.tz