Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndio sababu za serikali kukataza maandamano (+video)

Video Archive
Mon, 26 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa wanazuia kuwepo kwa maandamano ili kutoruhusu watu wachache wanaotamani Tanzania wavurugane na kuharibu taswira ya nchi.



Akizungumza jana katika Harambee iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Masaka dayosisi ya Pare, wilayani Same, alisema kuwa katika maandamano hayo wapo watu watakaofanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.

‘’Wapo wanaotamani tuvurugane na tunapowaeleza wananchi wanaweza kujiuliza kwanini tunazuia maandamano wakati wapo watu wanaofanya mazoezi na ni kwa sababu hatutaki kuruhusu watu watuburuge,’’ alisema Dkt. Mwigulu.

Chanzo: bongo5.com