Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hayati Dk Magufuli alimshawishi Mkapa kuacha utegemezi

696462ba0003c26463e0f9aae4e6113c Hayati Dk Magufuli alimshawishi Mkapa kuacha utegemezi

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

HAYATI Rais Dk John Pombe Magufuli anazungumziwa kama mtu mwenye uthubutu na ushawishi mkubwa ambapo alimshawishi Hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya ndani na kuachana na utegemezi wa fedha kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Isack Kamwelwe ambapo amesema ushawishi wake ulimfanya Mkapa kutengua kanuni za upatikanaji wa fedha za miradi mikubwa za (IMF).

“Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi wakati huo alimshawishi Mkapa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani, jambo ambalo halikuruhusiwa na shirika hilo.” amesema Kamwelwe.

"IMF ilikuwa inadhibiti na kusimamia matumizi ya fedha katika nchi maskini ikiwemo Tanzania, walikuwa wanatupimia namna ya kutumia fedha, mpaka kufikia mwaka 2000 tulikuwa haturuhusiwi kufanya miradi ya maendeleo kwa fedha zetu, tulikuwa tunapewa ruzuku kutoka IMF," aliongeza.

Alisema “Ushawishi wa Magufuli ulimwingia Mkapa akakubali kufuata ushauri wake ambapo alikaa na baraza la mawaziri na kupitisha azimio la kutenga Sh bilioni 1.8 kila mwezi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo."

Alisema hapo ndipo Tanzania ilitengua kanuni hiyo ya IMF na kuanza kujenga barabara, kuboresha miundombinu ya afya na miradi mingine ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu kwa kutumia fedha za ndani pamoja na ruzuku iliyokuwa ikitolewa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz