Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Hatuendekezi ujambazi, ukitoka aga kabisa" IGP Sirro mbele ya JPM (+video)

Video Archive
Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, amewataka wale wote wanaofanya uhalifu kwa kutumia silaha kuhakikisha kabla hawajatoka majumbani mwao wahakikishe wameziaga familia zao kwani jeshi hilo haliwezi kuwavumilia.

Kauli hiyo ameito mara baada ya Rais Magufuli, kuzindua Chuo cha Maafisa wa Polisi Kurasini Dar es Salaam.

“Watanzania na wahalifu watuelewe awamu hii si ya kuendekeza ujambazi wa kutumia silaha na ugaidi, ukiingia kwenye hii biashara usiilaumu serikali, kwahiyo Mh. Rais nikuhakikishie wale ambao hawataki kubadilika tutawalazimisha,” IGP Sirro

“Huwa nasema kabla hujachukua bunduki yako nyumbani kwako kwenda kusumbua Watanzania uage familia yako kwa sababu habari ya bunduki ukamataji wake huwa ni mgumu, Watanzania walishasahau benki zao kunyang’anywa fedha” IGP Sirro

LIVE : IGP SIRRO MBELE YA JPM “AWAMU HII SIO AWAMU YA UGAIDI, UJAMBAZI, MWANAMKE MTUNZE MMEO”

Chanzo: millardayo.com