Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halima Mdee ahoji uchafu Dar, Waziri Zungu aeleza mikakati

Video Archive
Fri, 31 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira nchini Tanzania, Mussa Zungu amesema dampo linalotumiwa na Jiji la Dar es Salaam lililopo Pugu Kinyamwezi lina hali mbaya.

Zungu ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 30, 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kawe, (Chadema), Halima Mdee.

 Halima ametaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kujenga dampo la kisasa jijini Dar es Salaam ili kutatua changamoto ya uchafu.

“Je Serikali ina mpango gani kujenga dampo la kisasa kwenye maeneo mengine kila wilaya ili kuzuia uchafu kutokana na lililopo kutokidhi kubeba uchafu katika jiji zima,” amehoji.

Akijibu swali hilo, Zungu amesema kasi ya taka katika jiji hilo ni kubwa licha linakua kwa kasi na kwamba miaka ijayo linakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni nane hadi tisa na dampo ni moja.

“Ni kweli hali ni ya uchafu, mbaya lakini nimwondoe hofu mbunge kuwa fedha zipo zimeshatolewa ili kujengwa la kisasa jipya ambalo litabeba taka zote katika jiji la Dar es Salaam,” amesema.

Pia Soma

Advertisement
Katika swali la msingi, Halima amesema Jiji la Dar es Salaam limekabiliwa na tatizo sugu la uchimbaji mchanga na uchafuzi uliokithiri.

”Serikali ina mikakati gani ya muda mfupi na mrefu kukabiliana na kero hii sugu na hatarishi,” amehoji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mussa Sima amekiri ni kweli kuna changamoto kubwa ya uchimbaji wa mchanga Dar es Salaam.

 Amesema ili kukabiliana na hilo hatua zinachukuliwa ni kuelimisha wananchi kuhusu athari za uchimbaji holela wa mchanga na kuzuia uchimbaji holela.

Chanzo: mwananchi.co.tz