Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haiwezekani mtu akisema haipendi CCM anatekwa, picha ya Rais inafungia chipsi - Mzee wa Upako

MZEE WA UPAKO Haiwezekani mtu akisema haipendi CCM anatekwa, picha ya Rais inafungia chipsi - Mzee wa Upako

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji wa Kanisa la Gospel Revival Center (GRC), Antony Lusekelo amehoji uwepo wa Matukio ya Watu kutekwa akidai inatokana na kutoa maoni yao na kueleza kuwa wanaofanya Vitendo hivyo wanatakiwa kufuata Sheria

Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ amesema “Inawezekanaje leo Kijana kuandika Mtandaoni ‘siikubali CCM’, unamteka au unasikia kapotea, imekuwaje? Sheria zipo, kamata peleka Mahakamani Nchi inatulia”

Ameongeza kuwa Vitendo vya Utekaji vinasababisha hata wenye mawazo mazuri wataogopa kuyatoa kwa hofu ya kutekwa na kupotezwa, pia kama kuna Sheria za Utekaji basi ziwahusu wanaokula viapo na kushindwa kuvisimamia.

“Haiwezekani leo kijana ameandika mtandaoni tu kwamba ‘siikubali CCM’, unamteka, unasikia kapotea, how comes? Sheria zipo, kamata peleka mahakamani, watu lazima waseme nchi yao kwa sababu ukifanya vile hata mawazo mazuri watu wataogopa kuyatoa wakihofia kutekwa, unaleta taharuki.

“Sheria za utekaji na kupiga watu zimo hata kwenye Biblia lakini nani mlengwa? Mtu aliyechana tu picha ya Rais ndiyo mlengwa huyo? Na ameshitakiwa akalipa faini…. Picha ya Rais si ipo kwenye magazeti na wanafungia nyama na chipsi? Huo ni mfano mdogo tu.

“Asili ya watu ni kusema, ila mnaweka mipaka kwenye kusema kwao, usiri, utulivu, usalama wa nchi kwa ajili ya miaka ijayo,” amesema Mzee wa Upako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live