Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gwajima awaacha hoi Magufuli, Wabunge "acha mbwa wabweke" (+video)

Video Archive
Sat, 14 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi, Josephat Gwajima, kwa mara ya kwanza leo Bungeni kazungumza, ambapo amemshukuru Rais Magufuli kwa kumrahisishia kuingia Bungeni, ambapo pia amemsihi kuendelea kuchapa kazi badala ya kusikiliza kelele za watu wengine.

“Ukiwa unasafiri halafu ukawa unasimama kila mahali kumtupia mawe kila Mbwa anayebweka, hutofika safari yako,  Rais wacha mbwa wabweke tuendelee na safari yetu ya kutimiza ilani ya kurasa 303, waache wabweke kwa raha zao wewe kaza mwendo” Gwajima

“Sisi wabunge tulioingia Bungeni kwa mara ya kwanza ‘performance’ yako ya miaka mitano iliyopita imetubeba sisi kwenye majimbo yetu na bila shaka tumepata kura kupitia wewe, ulikuwa ndiyo tofali katika ushindi wetu, kuna sehemu hatukuhitaji kupiga kura tulitaja jina lako tu” Gwajima

“NAFURAHI KUWAONA WABUNGE WASANII”. MWANA FA, BABU TALE, KEISHA

Chanzo: millardayo.com