Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fatma Karume na mtoto wa Chacha Wangwe kutinga mahakamani kupinga wakurugenzi kusimamia Uchaguzi (+video)

Video Archive
Wed, 7 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Wakili Fatma Karume na Mtoto wa aliyekuwa Mbunge Tarime, Chacha Wangwe, Bob Wangwe wanafungua kesi mbili mahakama Kuu kupinga Wakurugenzi kusimamia uchaguzi nchini.



kufungua Kesi kupinga Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi

Akiongea na waandishi wa habari leo,Fatma amesema kuwa Tanzania sasa baadhi ya viongozi waliwahi kusikika wakijinadi kushinda uchaguzi hata kwa magoli ya mkono na kudai kuwa haki ya kura sasa inaonekana kama haina thamani.

Amesema kuwa “Chini ya Katiba yetu refalii wa masuala haya ni Tume ya Uchaguzi, Katiba inasema huyo refalii lazima awe mtu ambaye hayumo kwenye chama chochote cha kisiasa siyo Chadema, CCM wala CUF bali anatakiwa awe mtu ambaye si mwanachama wa chama chochote, kwa hiyo msimamizi wa uchaguzi ni marufuku kuwa chini ya chama chochote kwa mujibu wa Katiba yetu yaani kuna matatizo makubwa ya sheria hapa,” alisema Fatma Karume

Chanzo: bongo5.com