Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fatma Karume awafunda vijana ACT-Wazalendo

98440 Pic+fatma Fatma Karume awafunda vijana ACT-Wazalendo

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanasheria wa kujitegemea Fatma Karume amewaeleza vijana wa ngome ya chama ACT -Wazalendo kuwa  wasitamani  kushika dola akisema sio yao bali kazi ya chama cha siasa ni kuendesha Serikali. Mwanasheria huyo ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu amesema vijana ndio viongozi wa nchi watarajiwa kwa miaka ijayo akiwataka kutotamani hata siku moja kushika dola watakapopata ridhaa hiyo. Fatma ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Machi 9, 2020 wakati wa mkutano mkuu wa ngome ya vijana ya ACT- Wazalendo uliokuwa na lengo la kuchagua safu mpya ya viongozi watakaoongoza ngome hiyo kwa miaka mitano ijayo. “Kazi ya chama cha siasa ni kuendesha Serikali kwa mujibu wa sera walizotoa kwa wananchi pamoja kujenga unafuu kati yao Serikali na wananchi "Kuna tofauti kati ya dola na Serikali, dola inahodhi Serikali na mhimili yote ya Serikali wakati kazi ya chama cha siasa ni kuendesha Serikali. Siku ikitokea mmechukua Serikali na kuhodhi dola nitasimama kuwaponda eleweni hivyo," amesema Fatma. Awali akifungua mkutano huo, mwenyekiti wa kikosi kazi maalumu cha ngome ya Vijana ya ACT- Wazalendo, Bonifacia Mapunda amesema huo ndiyo mkutano mkuu wa kwanza wa kuchagua viongozi akisema wakati wote ngome hiyo ilikuwa ikiendeshwa na kikosi kazi.

Chanzo: mwananchi.co.tz