Baada ya Mahakama Kuu kuzuia hatua ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamati ya Mawakili kupinga uamuzi wake wa kurejesha jina la Fatma Karume katika nafasi ya mawakili wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Fatma Karume ameeleza kuhusu mkwamo wa utekelezaji wa maagizo ya majaji.
https://publish.twitter.com/?query=https%3A%2F%2Ftwitter.com%2Ffatma_karume%2Fstatus%2F1472901395309379586&widget=Tweet
UKWELI ni huu. Majaji 3 wa Mahakama Kuu walibatilisha maamuzi ya TUME ya Nidhamu yakunifuta uwakil. Nikamuomba Sarwatt Msajili wa Mahakama Kuu kunirejeshea uwakili. Akakataa kwa sababu hizi 2:
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) December 20, 2021
1. Maamuzi ya Feleshi hayajabatilishwa na lazima niombe kama mtu aliyetiwa hatiani
2. Serikali imekata rufaa maamuzi ya TUME ya Nidhamu.
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) December 20, 2021
Sarwatt kakataa kunirejeshea UWAKILI kwa sababu hizo mbili.
Barua yake hiyo hapa.
Kwa hivyo eleweni, hata Msajili wa Mahakama Kuu haheshimu maamuzi ya majaji 3. Huu utamaduni wakudharau maamuzi ya majaji Uko mpaka Mahakamani pic.twitter.com/nvQzTmFYyr
Kwa hivyo eleweni, VIONGOZI wa Mahakama wameamuwa hawataki kuheshimu MAAMUZI ya Mahakama. Hawataki kunirejeshea UWAKILI.
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) December 20, 2021
Uwamuzi wa Serikali kukata rufaa haubatilishi HUKUMU ya Majaji 3. Lakini Msajili, kaamua yeye anaweza kudharau hukumu kwa sababu Serikali imekata rufaa!
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa malalamiko husika yaliwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kinyume na amri hiyo. Kwa hiyo, katika hukumu yao, majaji hao walimtaka Msajili wa Mahakama Kuu kupeleka malalamiko ya utovu wa nidhamu wa Bibi Karume kwa Kamati ya Mawakili kwa utaratibu ulioelekezwa katika amri ya Mahakama iliyotolewa na Jaji Mkuu wa wakati huo, Dk Eliezer Feleshi.
Kufuatia uamuzi wa jopo hilo, Wakili Fatma Karume aliendelea kusimamishwa kazi kwa mujibu wa amri ya Jaji Mkuu, akisubiri uamuzi wa Kamati, baada ya kupokea malalamiko mapya.