Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Tulia atembelea kaburi la Magufuli

Magufuli Kaburi Dkt. Tulia atembelea kabiri la Magufuli

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Tulia Ackson, amemtembelea na kuzungumza na mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli nyumbani kwake wilayani Chato mkoani Geita.

Dkt. Tulia pia ametembelea kaburi la Hayati Magufuli na kujumuika katika maombi mafupi pamoja na Mama Magufuli, aliyekuwa Mnikulu wa Hayati Magufuli na msemaji wa familia ya Magufuli ambaye kwa sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike.

Mwingine aliyejumuika ni Waziri wa Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Kapteni George Mkuchika ambapo tukio hilo limefanyika leo Jumatano, Machi 16, 2022.

Ikumbukwe kuwa, kesho Alhamisi, Machi 17, 2022 Hayati Magufuli anatimiza mwaka mmoja tangu alipofariki dunia katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matatizo kutokana na maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa miaka mingi.



Shughuli ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu atutoke pamoja na kumuenzi itafanyika Chato na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa mgeni rasmi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live