Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt Mollel aonya matumizi ya viungo vya binadamu katika tiba asili

Dkt Mollel Aonya Matumizi Ya Viungo Vya Binadamu Katika Tiba Asili.png Dkt Mollel aonya matumizi ya viungo vya binadamu katika tiba asili

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amewataka wataalamu wa tiba asili nchini kuacha matumizi ya viungo vya binadamu na wanyama katika huduma zao, akisisitiza kuwa dhana potofu zinazohusisha ngozi ya nyati, simba na mkia wa nyumbu zinapaswa kukemewa vikali.

Dk Mollel ametoa wito huo katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili Kitaifa jijini Mwanza Agosti 31, 2024 yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya chini ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

“Tunahitaji kuondokana na imani hizi potofu, ili kunusuru maisha ya wanyama pamoja na binadamu. Hakuna sababu ya kuendeleza matumizi haya ya viungo vya wanyama kwa kuwa ni hatari kwa mazingira na ustawi wa binadamu. Sisi sote tunapaswa kukemea vitendo hivi, kulinda mazingira na kuhakikisha tunafichua wenye vitendo viovu,” amesema Dk. Mollel.

Aidha, ameitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya tafiti za kina kwa wataalamu wa tiba asili, kwani NIMR inapaswa kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya dawa zinazotumika na kuhakikishazinatunzwa vizuri na kuendelea kuzalishwa kwa wingi.

Kwa upande mwingine, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Ahmad Makuwani, amekiri kuwa dawa zinazozalishwa na wataalamu wa tiba asili zimefanya maendeleo makubwa, huku mataifa mengine kama Angola yakizisajili kama dawa rasmi kwa matumizi ya binadamu.

Kilele cha maadhimisho hayo kimewakutanisha waganga wa jadi na wataalamu wa tiba asili, huku kikiwa na lengo la kuboresha huduma za tiba asili na kutetea haki za wanyama katika utendaji wa tiba hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live