alozi Dk Wilbroad Slaa anatarajiwa kuongoza kongamano la tafakuri tunduizi ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha hayati John Pombe Magufuli.
Kongamano hilo litakalofanyika Ijumaa Machi 25, mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), pia linalenga kufanya tafakuri ya miaka sita ya utekelezaji wa falsafa aliyoitumia hayati Magufuli wakati akiomba ridhaa ya kuiongoza nchi 2015.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Mwanza, Profesa Costa Mahalu ametaja wazungumzaji wengine katika kongamano hilo kuwa ni Mbunge Mstaafu wa Bariadi Mashariki, John Shibuda na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza.
Wengine ni wahadhiri na watafiti wabobezi wa Historia na Uchumi katika chuo hicho, Profesa Mihanjo Eginald na Dk Anne Gongwe.
"Wakati wa uchaguzi mwaka 2015, tulisikia CCM ikitumia slogani ya Magufuli for Change huku Chadema ikitumia- Movement for Change, kongamano hili litaenda kutafakari utekelezaji kwa vitendo vya slogan hizo," amesema Profesa Mahalu
Advertisement Profesa Mahalu amewaomba wasomi, wanataaluma na watanzania kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo ili kutoa mchango wao wakati huu ambao nchi inafanya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha Hayati John Magufuli na mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.