Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dada wa kazi aliyedaiwa kumchinja mtoto wa bosi wake akamatwa - VIDEO

Dada Wa Kazi Aliyedaiwa Kumchinja Mtoto Wa Bosi Wake Akamatwa.png Dada wa kazi aliyedaiwa kumchinja mtoto wa bosi wake akamatwa

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tarehe 17 Julai, 2024 lilitoa taarifa kuhusu dada wa kazi kufanya tukio baya la kikatili la kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni mtoto Malick Hashim (6) anayeishi eneo la Goba Kinzudi, Kinondoni.

Baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia. Upelelezi wa tukio hilo la kikatili ulianza mara moja na tarehe 21 Julai 2024 saa 4:00 usiku Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo aliyekuwa mfanyakazi wa nyumba wa ndani aitwaye Clemensia Cosmas Mirembe (19) akiwa amejificha kwenye “pagala” maeneo ya Goba Kizudi Kinondoni.

Mtuhumiwa huyo anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria.

Wito wetu Jeshi la Polisi ni kuwa pamoja na jitihada ambazo zinaendelea za kuzuia vitendo vya kihalifu tunawashauri wazazi, walezi, walimu, na jamii kwa ujumla kuwafundisha watoto kujenga tabia ya kutembea katika makundi lakini pia watoto wasikubali kuwakaribu na watu wasiowafahamu, watoto wasitumwe maeneo ambayo kwa mazingira ni hatarishi ikiwa ni pamoja na kuacha kuwatuma watoto wadogo maeneo mbalimbali nyakati za usiku.

Hata hivyo usalama katika jiji la Dar es Salaam umeimarishwa kwenye maeneo mbalimbali na Jeshi la Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam linaendelea kushirikiana na vyombo mbalimbali vya dola na wananchi kwa ujumla ili kundeleza jitihada zake za kuzuia vitendo vya kihalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live