Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chumi amrithi Balozi Mbarouk

Chumi Amrithi Balozi Mbarouk.png Chumi amrithi Balozi Mbarouk

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cossato Chumi ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi.

Mapema jana Jumapili Julai 21, 2024 Balozi Mbarouk ametangaza kujiuzulu ubunge. Taarifa za kujiuzulu kwake zimetolewa na Ofisi ya Bunge la Tanzania.

Taarifa hiyo ya Bunge imemnukuu Balozi Mbarouk akisema:"Ninalazimika kuchukua uamuzi wa kujiuzulu ili nipate nafasi ya kushughulikia changamoto hizo."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live