Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cherehani aomba Mkoa wa Tanesco Kahama

Cherehani Mbunge Sf.jpeg Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwka 2023/24 amemuomba Waziri wa Nishati January Makamba kumwelekeza mkandarasi wa kusambaza umeme katika Halmashauri ya Ushetu.

Cherehani amesema hiyo itaongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya umeme ili kutatua kero ya ukosefu wa umeme katika vijiji vilivyopo ndani ya halmashauri hiyo.

Mbunge huyo ametoa ombi hilo leo Alhamisi, Juni 1, 2023 Bungeni jijini Dodoma na kubainisha baadhi ya maeneo muhimu yenye kero kubwa ya umeme katika jimbo lake.

“Mkandarasi wako yupo taratibu sana, geografia ya Ushetu na vijiji vya Ushetu ni kubwa sana akaze buti ukiangalia majimbo yetu matatu na halmashauri tatu, msukumeni sasa akimbize vijiji vinahitaji umeme.

"Shule zinahitaji umeme, hospitali zinahitaji umeme na zahanati zetu zinahitaji umeme akimbize akamilishe hivyo vijiji 41 viweze kufikiwa umeme,” amesema Mbunge Cherehani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: