Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila amgusa Kiboko ya Wachawi, aonya vituo holela vya upandikizaji mimba

Chalamila Amgusa Kiboko Ya Wachawi, Aonya Vituo Holela Vya Upandikizaji Mimba.png Chalamila amgusa Kiboko ya Wachawi, aonya vituo holela vya upandikizaji mimba

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila ameonya kuhusu uanzishwaji holela wa vituo vya kupandikiza mimba kwa wanawake akisisitiza Wizara ya Afya inapaswa kuvidhibiti kuepuka wananchi kutapeliwa akitolea mfano huduma ya Kanisa la Christian Life Church.

Kanisa hilo lilikuwa likiongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe, maarufu Kiboko ya Wachawi, lililokuwa Buza Kwa Lulenge, jijini Dar es Salaam ambapo Julai 2024, Serikali ya Tanzania ilitangaza kulifunga kutokana na kwenda kinyume na taratibu za usajili.

Leo Alhamisi, Septemba 12, 2024 katika uzinduzi wa kituo cha upandikizaji mimba, gari la tiba kwa njia ya mkoba na kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam unaofanywa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Chalamila akazungumza hayo.

Chalamila amegusia utapeli huo akitolewa mfano usajili wa kanisa hilo ambalo lilikimbiliwa na wananchi na kubainika huduma zake haikuwa sahihi.

"Kulikuwa na kanisa lililokuwa maarufu ambalo hivi karibuni tulilifunga na aliyewasajili ni sisi na tulioona halifai ni sisi, ni kama tulijitekenya na kucheka wenyewe," amesema.

Chalamila amesema hata uanzishwaji wa kituo cha kupandikiza mimba kwa wanawake lazima watajitokeza watu wengi kutoa huduma hiyo kinyume na utaratibu hivyo Wizara ya Afya ni lazima idhibiti utoaji wa huduma hiyo kuepusha wananchi kutapeliwa.

"Kuwe na kasi ya udhibiti ili kuwe na ubora wa huduma," amesema Chalamila

Mbali na hiyo, Chalamila amesema kumekuwa na wananchi wengi wanafika ofisini kwake kwa malalamiko ya miili ya ndugu zao kuzuiwa hospitali kutokana na kutokamilisha gharama.

Amesema kumekuwa na maelezo mbalimbali juu ya hospitali kutozuia maiti hivyo ni muhimu tamko hilo liwe sheria ili kuepuka kuchonganisha wataalamu na ndugu wanaofata miili ya wapendwa wao hospitali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live